Mkurugenzi
wa world Vision hapa nchini Bwana Lugaimukamu akifafanua jambo katika mkutano
na waandishi wa habari leo juu ya maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji wa maziwa
ya mama duniani ambapo mwaka huu imejikita zaidi katika kuangalia maendeleo
yaliyofikiwa katika utekelezaji wa mkakati wa dunia kuhusu Ulishaji wa watoto
maziwa ya mama tangu kuzaliwa mpaka anapotimiza umri wa miaka sita uliodhinishwa na Shirika la Afya duniani (WHO) na Shirika la kuhudumia watoto
Duniani (UNSEF) miaka kumi iliyopita. Kulia kwake ni Bwana Joshua na Onesmo
Mella ambae ni kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe (TFNC) na kushoto
kwake ni Bibi Itika Kisunga mkurugezi wa Tanzania Consortium of Nutritionists
wakimsikiliza.
Mratibu wa
Lishe katika shirika la World vision nchini Bibi, Debora Mheya, ikielezea
baadhi ya mambo yatakayofanyika katika katika wiki hii ya unyonyeshaji wa
maziwa ya mama duniani kuwa ni pamoja na kutoa elimu mbalimbali juu ya maswala ya jinsi ya
kumlisha mtoto pamoja na kutoa elimu juu
ya tafiti mbalimbali zilizofanyika ambazo zinaonyesha kuwa hapa nchini
asilimia 49 ya watoto waliozaliwa wana anza kunyonyeshwa ndani ya saa moja baada
ya kuzaliwa. Huku watoto zaidi ya asilimia 94 uanza kunyonyeshwa ndani ya siku
ya kwanza baada ya kuzaliwa. Kulia
kwake Mratibu walishe ya watoto (TFNC) Bibi Neema Joshua na Onesmo Mella ambae
ni kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe (TFNC).