Tuesday, 31 July 2012

SAKATA LA KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANAHALISI


       Mkurugenzi wa mtendaji wa Hali Halisi Publishers Limited wachapishaji wa gazeti la MwanaHalisi bwana Saed Kubenea, amesema amesikitishwa na kitendo cha serikali kuendelea kutumia sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo ni mbaya na kandamizi kuyafungia magazeti nchini katika mkutano wake na waandishi wa habari mapema hii leo, kufatia kufungiwa kwa muda usiojulikana kwa gazeti la MwanaHalisi taarifa iliyotolewa jana na serikali kupitia Idara ya habari maelezo.
.
 
      Bwana kubenea amesema sheria hiyo katili ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo bado ipo hai,Haijafutwa watawala wanahitaji kuitumia kutunyang’anya Uhuru wa kufukiri, Uhuru wa kotoa maoni na Uhuru wa kuwasiliana na kutishia kufanya hivyo kwa vyombo vingine vya habari kitendo ambacho amekitafsili kuwa ni kitendo cha hatari
2    ivyo kuitaka serikali iondoe amri yake ya kulifungia gazeti la mwanahalisi na kutoa wito kwa wadau wengine wa habari kuwa wamoja katika kudai Uhuru na haki yetu ya kutafuta na kusambaza Habari.

No comments:

Post a Comment