Tuesday, 31 July 2012

MAADHIMISHO YA 20 YA WIKI YA UNYONYESHAJI MAZIWA YA MAMA DUNIANI


Mkurugenzi wa world Vision hapa nchini Bwana Lugaimukamu akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari leo juu ya maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji wa maziwa ya mama duniani ambapo mwaka huu imejikita zaidi katika kuangalia maendeleo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa mkakati wa dunia kuhusu Ulishaji wa watoto maziwa ya mama tangu kuzaliwa mpaka anapotimiza umri wa miaka sita uliodhinishwa na Shirika la Afya duniani (WHO) na Shirika la kuhudumia watoto Duniani (UNSEF) miaka kumi iliyopita. Kulia kwake ni Bwana Joshua na Onesmo Mella ambae ni kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe (TFNC) na kushoto kwake ni Bibi Itika Kisunga mkurugezi wa Tanzania Consortium of Nutritionists wakimsikiliza.

 
Mratibu wa Lishe katika shirika la World vision nchini Bibi, Debora Mheya, ikielezea baadhi ya mambo yatakayofanyika katika katika wiki hii ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama duniani kuwa ni pamoja na kutoa elimu  mbalimbali juu ya maswala ya jinsi ya kumlisha mtoto  pamoja na kutoa elimu juu ya tafiti mbalimbali zilizofanyika ambazo zinaonyesha kuwa hapa nchini asilimia 49 ya watoto waliozaliwa wana anza kunyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa. Huku watoto zaidi ya asilimia 94 uanza kunyonyeshwa ndani ya siku ya kwanza baada ya kuzaliwa.   Kulia kwake Mratibu walishe ya watoto (TFNC) Bibi Neema Joshua na Onesmo Mella ambae ni kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe (TFNC).

No comments:

Post a Comment