Source Mwananchi:
YUMKINI, wengi wanaposikia neno hili Loliondo akili zinaweza kuhamia kwa
Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapila, maarufu kama Babu aliyepata umaarufu
mwaka jana kwa kutibu maradhi mengi kwa dawa ya mitishamba iliyo katika
kikombe.
Lakini, Loliondo inayozungumziwa hapa si hiyo ya Babu wa Loliondo mkoani
Arusha. Loliondo hii haina kikombe cha babu wala haitibu kwa mitishamba, bali
ni eneo lililopo katika Kijiji Kichangani eneo la Kigamboni lenye upekee,
likiwa umbali wa kilomita 40 kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Upekee wake huo unatokana na majaliwa ya ardhi yenye rutuba tele na uoto
wa asili, lakini pia Kijiji cha Kichangani lilipo eneo la Loliondo lina
mchanganyiko wa watu wa makabila zaidi ya matatu, asilimia 70 wakiwa ni
Wasukuma.
Eneo hili lipo katika Kata ya Mbutu iliyopo Manispaa ya Temeke.
Baada ya kuvuka bahari kwa kutumia kivuko kutoka eneo la Kivukoni, yapo magari
mengi yanayoweza kukufikisha huko, ambayo wapigadebe wake hunadi maeneo
maarufu wanayopita na utawasikia wapigadebe hao wakiita abiria " Mbutu-
Kikwajuni – hadi Kichangani."
Ukishuka kituo cha mwisho wa gari, kinachoitwa Mbutu Kichangani, ukimuuliza
hata mtoto mdogo Loliondo ni wapi hapa? Atakupeleka.
Upekee mkubwa wa Loliondo ni kushamiri kwa biashara ya ukahaba, inayofanywa
na wasichana wa kuanzia umri wa miaka 13.
Loliondo ina nyumba zilizobatizwa jina la ‘ubanda’ na wenyeji wa eneo
wakimaanisha vibanda. Nyumba hizo ndimo inapofanyika biashara hiyo pamoja na
biashara ya kuuza pombe haramu ya gongo na bangi.
Wanawake wanaofanya biashara hiyo hapo Loliondo huitwa ‘wanawake wa ubanda’
Kwa nini eneo hilo likaitwa Loliondo?
Jina hilo linatokana na wanawake wanaotoa huduma ya ngono kuwaambia wanaume
wanaotaka kupata huduma yao: “Ngoja nikapate kikombe cha Babu Loliondo."
Ndipo jina hilo lilizaliwa na kutumiwa zaidi ya wanaume hao, wakijaribu kutumia
lugha ya kificho kwa safari ya kwenda huko, hata baadaye likakubalika na kuwa
maarufu.
Hamis Kashindye ni mkazi wa Kichangani, Loliondo, kwa miaka 16
sasa, anasema kuwa kama ingepitishwa sensa kujua idadi ya wanawake wanaouza
miili yao, basi wangeweza kuwa ni nusu ya wakazi wa eneo hilo.
Anasema kuwa wanawake hao wanaofanya biashara ya ukahaba baadhi ni wakazi
wa kudumu wa eneo hilo na wahamiaji kutoka maeneo ya Mbagala na Ilala.
“Hapa yapo mengi sana,(akimaanisha wanawake wanaojiuza) na kila siku
yanaongezeka. Wengine hawayapendi, lakini mimi naona yanasaidia sana,”
anasema Kashindye kwa lafudhi ya Kisukuma.
Anaitetea kauli yake kwa kueleza kuwa wapo wanaume wasioweza kutongoza
wanawake, hivyo wanarahisishiwa kazi kwa kutumia fedha zao kibindoni.
Anasema kuwa wanawake hao huwalenga wavuvi na wakulima wengine wa eneo hilo,
ambao baada ya kupata fedha zao huzitumia kwa starehe.
“Kama wavuvi na wakulima wa hapa wakishapata hela, wanamaliza hata
Sh100,000 kwa hao wanawake wa ubanda,” anasema Kashindye akifafanua kuwa baadhi
ya wanawake hao wana tabia ya kuhama hama wakifanya
No comments:
Post a Comment