Rais wa chama cha walimu Tanzania (CWT) Bwana Gration Mukoba
akitoa ufafanua kuhusu kushindikana kusuluhishwa na msuluhuishi
aliyeteuliwa na tume ya Usuluhishi na uamuzi juu ya mgogoro wake na
serikali juu ya madai yao katika mkutano wake na
waandishi wa habari jijini dar es salaam.kulia ni Mweka hazina wa
chama cha walimu Tanzania, kulia kwake ni mweka Hazina wa Chama cha walimu Bwana Mohamed Mutaly.
Rais wa chama Cha walimu Tanzania Bwana Gration Mukoba, akiwaonyesha
waandishi wa habari ( hawapo pichani) Cheti kilichotolewa na Msuluhishi
aliyeteuliwa na Tume ya Usuluhishi na Uhamuzi, kushindikana kufikia makubaliano cheti ambacho kimesainiwa na Msuluhishi ndugu Cosmas Fimbo baada ya kujadiliana kwa siku 30.
Kwa mujibu wa sheria kifungu cha 80-(1) cha sheria ya ajira na
mahusiano kazini ya mwaka 2004, Ivyo chama cha walimu tanzania kimetoa
wito kwa wanachama wake kuanzia jana tarehe 25/ 6/ 2012 kuanza kupia
kura ya NDIO au HAPANA kwa wanachama wake wote nchini ili kukubali
kugoma au kusiwepo na mgomo
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhulia mkutano huo, katika ofisi ya
Chama cha Walimu Tanzania makao makuu jijini dar es salaam, walimsiliza
kwa makini Rais wa chama cha walimu (hayupo pichani) hakitoa tamko juu
ya mgogoro huo na serikali baada kushindwa kufikia makubaliano kati yao.
No comments:
Post a Comment