Wednesday, 20 March 2013

BALOZI WA CANADA NCHINI ATEMBELEA SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN

Balozi wa CANADA nchini bwana, Alexandre Leveque katikati, katika mkutano na waandishi wa habari hawapo pichani, alipotembelea shirika la Under the Same Sun kwa lengo la kujionea utendaji wake pamoja na kuzindua vipindi vya kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu Albinisim, mradi ambao umefadhiliwa kwa ushirikiano wa serikali ya Canada kupitia ubalozi wake nchini na shirika la Under the Same Sun. kushoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa(UTSS) Bi,Vicky Ntetema.


Balozi wa Canada nchini Bwana Alexandre Leveque, akibonyeza kitufe akizindua vipindi vya kampeni Tambua Albinism inayotarajiwa kuanza mwezi wa April, Jumla ya vipindi kumi na mbili vyenye urefu wa dakika therathini, vya michezo wa radio na makala mchanganyiko zenye lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu albinism kama hali ya kurithi na changamoto zinazowakabili watu wenye albinism (WWA), vitarushwa katika radio za kijamii Sengerema Fm, Sibuka Fm, Faraja Fm, Fedeco Fm, Kahama Fm na Chemchemi Fm ziliopo kanda ya ziwa.

Balozi wa Canada nchini Bwana, Alexandre Leveque akikabidhi mfano wa hundi ya USD 20,000 kwa mkugenzi mtendaji wa UTSS Bibi Vicky Ntetema kushoto kwake ambazo zitasaidia kutekeleza kampeni hiyo yenye lango la kuamamsisha jamii juu yamaswala ya Albinism vipindi vitakavyorushwa hewani kwa mda wa miezi sita.
Vipindi viwili kwa mwenzi vya makala mchanganyiko vitarushwa na (kurudiwa), kipindi kimoja cha mchezo wa radio kitarushwa hewani mara moja kwa mwezi na (kurudiwa0 pia kutakuwa na jopo la majadiliano ya moja kwa moja pamoja na mazungumzo kati ya WWA, na wataalam wa maswala ya albinism sanjali na michango ya wasikilizaji wakaochangia kwa njia ya simu.
  


Tuesday, 19 March 2013

MPYA KUHUSU LUDOVICK RWEZAURA

Naomba sasa nieleze vipi ninavyomfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA nikishabihisha ufahamu wangu huo kwake na matukio yanayoendelea hivi sasa.

Katika mfululizo wa matukio yanayoendelea hapa nchini hasa yanayogusa medani za siasa za ndani ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla wake, katika yote lipo tukio moja ambalo ni kubwa na lenye sura ya kuogofya. Kwa kuwa tukio lenyewe lipo katika mchakato wa kimahamakama sitalizungumza bali nitazungumza nje ya Wigo wa kesi hiyo ili nisiingilie hatua za kimahakama na nisivunje sheria za nchi.

Nitakachokisema hapa ni namna tu ambavyo nimewahi kumfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA ambae ni mmoja wa washukiwa wa matukioyakigaidi.

Nilikutana na LUDOVICK pindi nilipokuwa Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Ualimu (BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION “BAED”) katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Campus ya DUCE mwaka 2008-9 nikiwa mwanafunzi wa Mwaka wa pili, LUDO akiwa mwaka wa kwanza.
Nikiwa ni miongoni mwa vijana wana mkakati na wapinaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nikiendesha shughuli mbalimbali za kukijenga na kukiimarisha Chama hiko katika maeneo ya Vyuo Vikuu, nikiwa nina wajibu na majukumu ya kuwashawishi vijana kujiunga na Chadema na kuwajengea imani na matumaini ya kupata Maisha mzuri na Ajira katika taasisi mbalimbali za kijamii zilizo affiliated na Chama hiko, ndipo nilipokutana na LUDO na kuzungumza nae kisha kuungana pamoja kuijenga chadema.(LUDO akiwa mwaka wa Kwanza akifanya BAED-history&political science)
Harakati zetu ziliendelea kwa mafanikio ambapo tulikuwa tukipanga na kufanikisha mikakati mbalimbali ya kuandaa matukio na mijadala ambayo tulialika vongozi wakuu wa Chadema kuja kuzungumza issues mbalimbali za kitaifa na kichama.
Katikati ya Mwaka 2009 nilipata wazo la kuanzisha Jumuiya ya wanafunzi chini ya Chadema, ambapo CHASO ilizaliwa, nikiwa ni muasisi na “mwanzilishi pekee” wa Jumuiya hiyo ya CHADEMA STUDENTS ORGANISATION (CHASO), Ilianza kazi rasmi ya kuwaweka pamoja wanafunzi wanachama wa Chadema mimi Nikiwa ni MWENYEKITI wa kwanza wa jumuiya hiyo. Tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kuwashawishi wanafunzi wengi kujiunga na Chadema, haya tuliyafanya PAMOJA. Hata ilipofika mwaka 2010 niling’atuka kama Mwenyekiti na kuiacha jumuiya hiyo katika mikono salama ya LUDOVICK, ambapo aliendelea nayo jumuiya mpaka Mwaka 2011, alipokuwa Mwaka wa Mwisho naye alikabidhi Uenyekiti kwa Peter John shughuli ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa TTC Chang’ombe na mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Slaa ambapo aliambatana na Dr. Azaveli Lwaitama-mhadhiri wa UDSM.
Baada ya kuhitimu chuo, LUDO alikuja Makao Makuu ya Chadema kama Volunteer ambapo alijumuika tena na volunteer wengine (mimi nikiwemo tangu mwaka 2008) ambapo LUDO alipewa kazi ya kupambana ndani ya mitandao ya kijamii (ikiwemo JF kwa ID ya MPEPO)
Ilipofika Mwanzoni mwa Mwaka 2012, LUDO alikuwa amepangiwa TABORA kama Mwalimu wa Sekondari ambapo LUDO alikwenda kuanza maisha mapya ya kufundisha , ambapo Mwezi mmoja tu baadae Dr. Slaa alimuita arudi Makao Makuu na kumuweka katika Idara ya Ulinzi na Usalama, Chini ya WILFRED LWAKATARE.
Nitaeleza kwa ufupi kwanini Dr Slaa alimpa LUDO kazi hiyo:-
i) LUDOVICK alisoma shule ya seminary na pia alisoma masomo ya Uchungaji kwa miaka minne, hivyo alikuwa ni mtiifu sana kwa Dr SLAA na pia aliamini amesoma kwa undani mafunzo ya kutunza siri na uaminifu.
ii) Pia LUDO alikuwa akiwa ni mtu anayepeleka taarifa kwa Dr SLAA kuhusu viongozi wengine ndani ya Chadema na pia alikuwa akitumika katika mitandao ya kijamii kuwashughulikia viongozi wengine wa Chadema.(Pindi alipokuwa kitengo cha mitandao ya Kijamii)
iii) Credit nyingine aliyoipata kwa Dr Slaa ni pale alipopeleka majina ya wagombea wa BAVICHA ambao wamekataa kutumika na Dr Slaa (Mimi nikiwemo) na kupelekea majina yetu kuenguliwa, Uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika pale ukumbi wa P.T.A sabasaba.
iv) Lakini pia LUDO aliaminika pia na LWAKATARE kwa kuwa walitoka Mkoa mmoja wa Kagera.
Hivyo, Mwaka 2012 LUDO alikuwa miongoni mwa frontline Undercover katika chaguzi mbalimbali, ambapo alitumikia pia kama afisa usalama wa Viongozi wa Juu wa Chama, ambapo aliongozana na DR SLAA kama mlinzi wake kuelekea kwenye Uchaguzi wa JIMBO la UZINI kule ZANZIBAR.
Aliendelea na nafasi yake hiyo katika Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya Chadema kwa kupanga ba kufanikisha mikakati mbalimbali, ambapo nilikutana nae Big Brother mwanzoni mwa Mwaka huu, alikuwa anatoka PACIFIC HOTEL akaniambia kuwa ametoka MBOZI MAGHARIBI ambako alikwenda kuchunguza kama DAVID SILINDE anakubalika jimboni kwake, na hata ilipotokea sakata lililopelekea Mimi na SHONZA na wengineo kuondoka Chadema, LUDOVICK ndiye mtu aliyetumwa kwenda MBEYA akiwa na maagizo kutoka kwa DR SLAA ya kumfukuza UANACHAMA baba yangu Mzazi (MZEE MWAMPAMBA ambae nae alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA) na ndiye aliyekuja hapa jamiiforums (JF) kuweka post yenye barua za kufukuzwa kwa Mzee Mwampamba.
PAMOJA NA HAYA YOTE NA MENGINE AMBAYO AMEIFANYIA CHADEMA AMBAYO MIMI SIYAJUI, VIONGOZI WA CHADEMA WANAKANA KUMFAHAMU……….,INAHUZUNISHA..!
Nimeshtushwa sana na Taarifa nilizoziona kwenye vyombo vya habari, juu ya Dr SLAA kukana kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia na kufanya nae kazi yeyote NDUGU yangu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA.
Lakini si hilo tu bali pia Mawakili ambao wamewekwa na Chadema ambao idadi yao ni watano, wakiwemo (katika mawakili hao) viongozi waandamizi wa Chadema wamekana kumtambua LUDOVICK.,ni USALITI KIASI GANI HUU..?
Mawakili wote watano ambao ni:-
i) MABERE MARANDO-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
ii) ABDALLAH SAFARI-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
iii) NYARONYO KICHERE
iv) TUNDU LISSU-MNADHIMU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI
v) PETER KIBATALA
Kwanini wasigawanywe hawa au wote katika hawa hawamtetei LUDO..? ama kama si hawa kwanini hawatafutwi mawakili wengine kwa ajili ya LUDO na badala yake akaachwa anaangamia pamoja na kujitolea kote kuijenga na kuitetea Chadema, pamoja na utiifu wote wa kuwalinda na kutunza siri za viongozi na siri za Chama hicho.
ANGALIZO:
Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na upepo wa mawazo yao.
Naomba vijana wenzangu mfikiri kwa kina juu ya haya yaliyompata LUDOVICK na mjifikirie hatma yenu ndani ya chama na maisha katika ujumla wake.

CHANZO" MTELA MWAMPAMBA/ FACEBOOK

Sunday, 17 March 2013

HATIMAE JESHI LA POLISI KUTOA MAELEZO JUU YA SAKATA KIBANDA KESHO

Hatimaye sakata la kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, (TEF), Absalom Kibanda, limepata mwanga na watuhumiwa wa kadhia hiyo wataanikwa hadharani kesho.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema timu iliyoundwa kuchunguza kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Kibanda, itatoa taarifa kamili na idadi ya watu waliowakamata kuhusiana na tukio hilo.

Wakati Kova akieleza hilo, mitandao ya kijamii jana ilieleza kuhusu taarifa za kukamatwa kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Ludovick Joseph kwa tuhuma za kuhusika kuteswa kwa Kibanda.

Kova alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo, aliomba apewe muda ili awasiliane na mwenyekiti wa timu iliyoundwa kuchunguza tukio hilo.

“Tangu asubuhi nilikuwa Mabwepande, ndiyo nimerudi ofisini muda sio mrefu, kuhusu hilo nimelisikia kupitia kwa waandishi wenzako walionipigia simu, nipe muda nilifuatilie,” alisema.

Baada ya kupigiwa tena, Kova alisema kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa na timu hiyo, haikuwa muda muafaka kulizungumzia suala hilo jana.

“Wameniambia taarifa kamili ya kile walichokuwa wakikichunguza kwa muda wote, kitatolewa siku ya Jumatatu (kesho) kupitia mkutano wa waandishi wa habari. Huko mtaelezwa wangapi walikamatwa na kuhojiwa na nini kitafuata,” alisema Kova na kukata simu.
Awali, taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilieleza kuwa, Joseph alikamatwa akiwa mkoani Iringa.

Gazeti hili lilipowasiliana na Kaimu Kamanda wa mkoa huo, Wankyo Nyigesa, alisema tangu juzi amekuwa akipokea simu za waandishi wa habari zikiulizia tukio hilo.

Alisema amewasiliana na polisi kwenye eneo lake na kuthibitishiwa hakuna tukio la aina hiyo na kumwomba mwandishi ajaribu kuwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe.

Kupitia mtandano wa kijamii wa ‘Mjengwa’, katika ukurasa wake aliandika kuwa usiku (bila kutaja ni lini) akiwa kwenye shughuli ya shule ya watoto wake Highlands Hall Iringa, alipata habari kuwa Joseph amekamatwa.

Katika ukurasa huo alidai kuwa Joseph alikamatwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kuhusika na kuteswa mwandishi Absalom Kibanda.

Pia alidai jinsi anavyomfahamu kijana huyo toka akiwa Chuo Kikuu (DUCE) na kwamba ni mmoja wa Watanzania anaowafahamu kupitia kazi zake za magazeti.

Taarifa hiyo ilisema, Joseph amekuwa akiishi Dar es Salaam na ni miongoni mwa waliokuwa wakimsaidia kwa kujitolea kwenye kazi zake za mitandaoni, hususan kwenye Mjengwablog na website (tovuti) ya kwanza ya Jamii.

Kadhalika, alisema miezi ya hivi karibuni Joseph ndiye aliyekuwa akifanya kazi ya kuingiza magazeti kwenye Mjengwa blog kila asubuhi.

“Akiwa Dar es Salaam na mimi nikiwa Iringa, Ludovick hakuwa mwajiriwa wangu kama wanavyodhani wengine, bali amekuwa ni mmoja wa vijana waliokuwa tayari kunisaidia kwa kazi za hapa na pale ikiwamo kunipelekea invoice (ankara ya malipo) kwa watangazaji kwenye Mjengwa blog. Mara nyingi nimekuwa nikimtambulisha kama ' Msaidizi wa Mwenyekiti” alisema.

Aliongeza kuwa juzi alimwomba aende Iringa ampelekee vitabu vyake vya invoice na risiti kutokana na kutegemea ugeni kutoka Mfuko wa Ruzuku kwa Vyombo vya Habari (TMF).
Mjengwa blog katika ukurasa huo, amedai kuwa katika hilo lililomtokea, hawezi kumtetea wala kumtia hatiani kwa kuwa naye ni binadamu kama wengine na hawezi kusema anamfahamu zaidi.

“Kwa vile yuko mikononi mwa vyombo vya usalama, nina imani, kuwa vyombo hivyo vitafanya kazi yake ili kutusaidia katika kupata ukweli wa jambo zima…”

“Na kama ni kweli kwa namna yoyote ile itathibitishwa kuwa ameshiriki njama za kupanga mikakati hiyo ya kigaidi, basi, ahukumiwe kwa dhambi hiyo,” alisema.

Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006), alijeruhiwa usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita na watu wasiofahamika.  





                                    
 Source: NIPASHE


Friday, 15 March 2013

JUMLA WASHIRKI 66 KUSHINDANA TUZO (EJAT) 2012.

                         TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Baraza la habari Tanzania (MCT), leo limetangaza majina ya waandishi wa habari wateule watakaoshiriki katika Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2012 zitazotolewa tarehe 5 April 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, ilyotolewa na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa tunzo za (EJAT) 2012, Bwana kajubi Mukajanga imesema kuanzi tarehe 25 Feb 2011 hadi 3 March 2013, jumla kazi 946 ziliwakilishwa na waandishi kushindanishwa, Idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Kazi hizo zikipitwa ili kuwapata wateule hao, ambapo jopo la majaji tisa likiongozwa na Bi, Benardina Chahali Mhariri mkuu wa Kituo cha Televisheni ya Chanel Ten, lilipitia kazi hizo na kupata wateule wa tunzo hizo kwa mwaka 2012, ambapo jumla ya wateule kutika Radio ni 18, Televisheni 16 na magazeti ni 32, ndio watashiriki katika Tuzo za (EJAT) mwaka 2012, kufanya jumla ya wateule kuwa watakaoshiki katika chuzo hizo kuwa 66, Toafauti na mwaka 2011 ambapo walikuwa 72.

Aidha taarifa hiyo imesema kuwa jopo la wataalamu lililoundwa kumtafuta mshindi wa tunzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tansia ya habari tayali limeshakabidhi majina ya wateule watatu ambayo mshindi atakabidhiwa Tuzo na Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein usiku wa tarehe 5 April 2013 katika Halfa ya kutoa tuzo hizo jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo majina ya wateule wa wa mshindi wa jumla ni.
Daniel Kaminyoge, faraja sendegeya, Lucas Liganga, Gervas Hubile, Florence Majani, Fred Azzah na Idd Juma Yusuph.
  




Thursday, 14 March 2013

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS DR, MOHAMED BILAL KATIKA WIZARA YA MAJI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Bwana Said mecky Said Akimkaribisha makamu wa Rais Dr MOHAMED BILAL, kuzindua kisima cha maji safi katika eneo la mji mpya la mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 


Mwakilishi wa kampuni ya kusambaza maji safi na maji taka jijini Dar es Salaam akitoa maelezo mafupi ya mradi wa kusambaza maji kwa makamu wa Rais Dr Mohamed G Bilal katika eneo la mabwepande nje kidogo ya jiji la dar es Salaam


Waziri wa Maji Prof Jumanne maghembe, Akimkaribisha mgeni rasmi makamu wa rais dr Mohamed G Bilal kuzungumza na wananchi wa eneo ilo pamoja na wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na maji taka  katika ziara yake ya kujionea hali ya maji nchi.


Mkamu wa rais Dr Mahamed G bilal akitoa nasaha zake kwa wananchi wa eneo hilo na kuwataka kutunza na kuakisha maji hayo yatumika vizuri ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku, pia ametoa wito kwa wananchi kuwataja wale wote wanaohujumu miundombinu ya maji pamoja na kujiunganishia kinyemela huduma hiyo ya maji ili waweze kuchuliwa hatua za kisheria.


Aidha makamu serikali inatambua kuwepo kwa changamoto katika upatikanaji wa majikubwa ni Ongezeko la idadi ya watu pamoja na mbadiliko ya tabia nchi yanayosababisha ukame na wakati mwimgine mafuriko ivyo serikali kupitia sera ya maji imejipanga kuzikabili changamoto hizo kwa kuwashirikisha pia na wadau mbalimbali.


 Baadhi ya Wananchi na wafanyakazi wa DAWASA na DAWASCO wakimsikiliza makamu wa Rais Dr Mohamed G Bilal hayupo pichani

Makamu wa rais Akipanda mti kama kumbukumbu baaada ya kuzindua kisima cha maji safi katika mji wa mabwepande nje ya jiji la Dar ers Salaam.


Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe nae akipamda mti wa kumbukumbu baada ya makamu wa rais Dr Mohamed G Bilal kuzindua kisima cha maji safi katika eneo la mabwepande  nje ya jiji la dar es salaam, katika ziara yake ya kukagua Hali ya maji nchi.







Wednesday, 13 March 2013

ZIARA YA MTENDAJI MKUU WA (NEPAD) MAKAO MAKUU YA TFDA



Mtendaji mkuu wa (NEPAD). Dr IBRAHIM ASSANE MAYAKI akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari awapo pichani mara baada ya kuwasili katika ofisi za mamlaka ya dawa na chakula (TFDA) leo,


Mkurugenzi mkuu wa (TFDA) Bwana HIITI SILLO, Pichani akimkabidhi mkurugenzi  mkuu wa (NEPAD), Dr IBRAHIM ASSANE MAYAKI, Tuzo kutambua mchango wake katika kuakikisha nchi za afrika hasa afrika mashariki zinakuwa na viwango sawa katika vya bidhaa lengo ni kusaidia kutokomeza bidhaa zisizokidhi viwango katika nchi hizo.


Baada ya kufanya dhiara na kujionea jinsi TFDA inavyofanya kazi zake katika vitengo mbalimbali, hakaitimisha ziara yake kwa kupiga picha ya pamoja na wafanyakazi 

PAPA MPYA NI KUTOKA ARGENTINA



CARDINAL JORGE MARIO BERGOGLIO KUTOKA NCHINI ARGENTINA  ACHAGULIWA KUWA PAPA MPYA, NA KUCHAGUA JINA LA FRANCIS 1

Monday, 11 March 2013

POLISI WATANO WALIOHUSIKA NA WIZI WA MIL 150 WAFUKUZWA KAZI


Askari watano SSGT Dancan, CPL Rajab, CPL Calvin, CPL Geofrey, na CPL kawanami wamefukuzwa kazi kitokana na makosa mbalimbali ya kinidhamu pamoja na kuhusika katika wizi wa Tsh 150 Milioni uliotokoea kariakoo tarehe 14 Dec mwaka jana.Akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam, Kamanda wa polisi kanda maalumu DCP Sulemani Kova amsema, askari hao watashitakiwa kwa kumujibu na taratibu za kijeshi ambapo zinataka askari yeyote kabla ya kushtakiwa mashtaka ya kiraia wanatakiwa kushitakiwa katika mahakama za kijeshi kwanza.Kamanda Kova ameongeza kuwa sambamba na kufukuzwa kazi jarada lao tayali limeshapelekwa katika ofisi ya DPP na ofisi  ya mwanasheria wa serikali ili waweze kulipitia na kuona kama kuna uwezekano wa washtakiwa hao kufikishwa katika mahakama za kawaida (Criminal Justice).


Pia Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanya Operetion ya kushtukiza jijini Dar es saaam, Na kufanikiwa kukamata Noti bandia za Elfu kumi Sita, Bastora iliyokuwa na risasi nane, Pikipiki aina ya Boxer yenye namba ya usajili T 639 CDS pamoja na watuhumiwa watau, lita 66 za pombe aina ya gongo, bangi, katika operation hiyo  jeshi ilo likifanikiwa kuwakamta watuhumiwa 35 kutokana na makosa hayo. 

MOAT KUZIMA MATANGAZO YA TV NCHINI


Chama cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini MOAT, kimeiomba serikali kurudisha mfumo wa kurusha matangazo ya anlojia kwa mda nchini kwani mfumo wa dijitali  unawanyima  wananchi wengi haki ya ya kikatiba ya kupata habari nchiniMwenyekiti wa MOAT, Bwana Reginard Mengi amesema tangu kuanza kwa mfumo huo wa kurusha matangazo wa dijitali nchi desemba31 mwaka jana, watu wengi hasa wa kipato cha chini nchini wamekuwa wakishinshindwa kupata haki yao ya kikatiba ya kupata habari  ivyo kusababisha vituo vingi vya kurusha matangazo ya tv kushindwa kufikia malengo yao kiutendaji.Ameongeza kuwa ktk kipindi icho chote kuanzia desemba 31 mwaka jana ambapo mfumo wa utangazaji wa analojia ulizimwa nchini na kuanza kutumika mfumo wa dijitali kumepelekea wadhamini wengi kusitisha matangazo yao au kuyapeleka ktk radio kutokana na kutokuwa na watazamaji wengi nchini wa tv, kwani wanaoweza kumiliki mfumo huo mpya wa dijitali.Aidha Bwana Mengi amebainisha kuwa kutokana na wadhamini wengi kusitisha kutoa matangazo yao  kutapelekea vituo vya kurusha matangazo ya tv vingi nchini kushindwa kujiendesha au kusitisha kurusha matangazo yake mda sio mrefu.