Waziri wa Maji Prof Jumanne maghembe, Akimkaribisha mgeni rasmi makamu wa rais dr Mohamed G Bilal kuzungumza na wananchi wa eneo ilo pamoja na wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na maji taka katika ziara yake ya kujionea hali ya maji nchi.
Mkamu wa rais Dr Mahamed G bilal akitoa nasaha zake kwa wananchi wa eneo hilo na kuwataka kutunza na kuakisha maji hayo yatumika vizuri ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku, pia ametoa wito kwa wananchi kuwataja wale wote wanaohujumu miundombinu ya maji pamoja na kujiunganishia kinyemela huduma hiyo ya maji ili waweze kuchuliwa hatua za kisheria.
Aidha makamu serikali inatambua kuwepo kwa changamoto katika upatikanaji wa majikubwa ni Ongezeko la idadi ya watu pamoja na mbadiliko ya tabia nchi yanayosababisha ukame na wakati mwimgine mafuriko ivyo serikali kupitia sera ya maji imejipanga kuzikabili changamoto hizo kwa kuwashirikisha pia na wadau mbalimbali.
Baadhi ya Wananchi na wafanyakazi wa DAWASA na DAWASCO wakimsikiliza makamu wa Rais Dr Mohamed G Bilal hayupo pichani
Makamu wa rais Akipanda mti kama kumbukumbu baaada ya kuzindua kisima cha maji safi katika mji wa mabwepande nje ya jiji la Dar ers Salaam.
Waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe nae akipamda mti wa kumbukumbu baada ya makamu wa rais Dr Mohamed G Bilal kuzindua kisima cha maji safi katika eneo la mabwepande nje ya jiji la dar es salaam, katika ziara yake ya kukagua Hali ya maji nchi.
No comments:
Post a Comment