Naomba sasa nieleze
vipi ninavyomfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA nikishabihisha ufahamu wangu huo
kwake na matukio yanayoendelea hivi sasa.
Katika mfululizo wa matukio yanayoendelea hapa nchini hasa yanayogusa medani za
siasa za ndani ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla wake, katika yote lipo tukio
moja ambalo ni kubwa na lenye sura ya kuogofya. Kwa kuwa tukio lenyewe lipo
katika mchakato wa kimahamakama sitalizungumza bali nitazungumza nje ya Wigo wa
kesi hiyo ili nisiingilie hatua za kimahakama na nisivunje sheria za nchi.
Nitakachokisema hapa ni namna tu ambavyo nimewahi kumfahamu LUDOVICK JOSEPH
RWEZAURA ambae ni mmoja wa washukiwa wa matukioyakigaidi.
Nilikutana na LUDOVICK pindi nilipokuwa Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya
Ualimu (BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION “BAED”) katika Chuo Kikuu cha Dar es
salaam (UDSM) Campus ya DUCE mwaka 2008-9 nikiwa mwanafunzi wa Mwaka wa pili,
LUDO akiwa mwaka wa kwanza.
Nikiwa ni miongoni mwa vijana wana mkakati na wapinaji wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) nikiendesha shughuli mbalimbali za kukijenga na
kukiimarisha Chama hiko katika maeneo ya Vyuo Vikuu, nikiwa nina wajibu na
majukumu ya kuwashawishi vijana kujiunga na Chadema na kuwajengea imani na
matumaini ya kupata Maisha mzuri na Ajira katika taasisi mbalimbali za kijamii
zilizo affiliated na Chama hiko, ndipo nilipokutana na LUDO na kuzungumza nae
kisha kuungana pamoja kuijenga chadema.(LUDO akiwa mwaka wa Kwanza akifanya
BAED-history&political science)
Harakati zetu ziliendelea kwa mafanikio ambapo tulikuwa tukipanga na
kufanikisha mikakati mbalimbali ya kuandaa matukio na mijadala ambayo tulialika
vongozi wakuu wa Chadema kuja kuzungumza issues mbalimbali za kitaifa na
kichama.
Katikati ya Mwaka 2009 nilipata wazo la kuanzisha Jumuiya ya wanafunzi chini ya
Chadema, ambapo CHASO ilizaliwa, nikiwa ni muasisi na “mwanzilishi pekee” wa
Jumuiya hiyo ya CHADEMA STUDENTS ORGANISATION (CHASO), Ilianza kazi rasmi ya
kuwaweka pamoja wanafunzi wanachama wa Chadema mimi Nikiwa ni MWENYEKITI wa
kwanza wa jumuiya hiyo. Tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kuwashawishi
wanafunzi wengi kujiunga na Chadema, haya tuliyafanya PAMOJA. Hata ilipofika
mwaka 2010 niling’atuka kama Mwenyekiti na kuiacha jumuiya hiyo katika mikono
salama ya LUDOVICK, ambapo aliendelea nayo jumuiya mpaka Mwaka 2011, alipokuwa
Mwaka wa Mwisho naye alikabidhi Uenyekiti kwa Peter John shughuli ambayo
ilifanyika katika Ukumbi wa TTC Chang’ombe na mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Slaa
ambapo aliambatana na Dr. Azaveli Lwaitama-mhadhiri wa UDSM.
Baada ya kuhitimu chuo, LUDO alikuja Makao Makuu ya Chadema kama Volunteer
ambapo alijumuika tena na volunteer wengine (mimi nikiwemo tangu mwaka 2008)
ambapo LUDO alipewa kazi ya kupambana ndani ya mitandao ya kijamii (ikiwemo JF
kwa ID ya MPEPO)
Ilipofika Mwanzoni mwa Mwaka 2012, LUDO alikuwa amepangiwa TABORA kama Mwalimu
wa Sekondari ambapo LUDO alikwenda kuanza maisha mapya ya kufundisha , ambapo
Mwezi mmoja tu baadae Dr. Slaa alimuita arudi Makao Makuu na kumuweka katika
Idara ya Ulinzi na Usalama, Chini ya WILFRED LWAKATARE.
Nitaeleza kwa ufupi kwanini Dr Slaa alimpa LUDO kazi hiyo:-
i) LUDOVICK alisoma shule ya seminary na pia alisoma masomo ya Uchungaji kwa
miaka minne, hivyo alikuwa ni mtiifu sana kwa Dr SLAA na pia aliamini amesoma
kwa undani mafunzo ya kutunza siri na uaminifu.
ii) Pia LUDO alikuwa akiwa ni mtu anayepeleka taarifa kwa Dr SLAA kuhusu
viongozi wengine ndani ya Chadema na pia alikuwa akitumika katika mitandao ya
kijamii kuwashughulikia viongozi wengine wa Chadema.(Pindi alipokuwa kitengo
cha mitandao ya Kijamii)
iii) Credit nyingine aliyoipata kwa Dr Slaa ni pale alipopeleka majina ya
wagombea wa BAVICHA ambao wamekataa kutumika na Dr Slaa (Mimi nikiwemo) na
kupelekea majina yetu kuenguliwa, Uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika pale ukumbi
wa P.T.A sabasaba.
iv) Lakini pia LUDO aliaminika pia na LWAKATARE kwa kuwa walitoka Mkoa mmoja wa
Kagera.
Hivyo, Mwaka 2012 LUDO alikuwa miongoni mwa frontline Undercover katika chaguzi
mbalimbali, ambapo alitumikia pia kama afisa usalama wa Viongozi wa Juu wa
Chama, ambapo aliongozana na DR SLAA kama mlinzi wake kuelekea kwenye Uchaguzi
wa JIMBO la UZINI kule ZANZIBAR.
Aliendelea na nafasi yake hiyo katika Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya Chadema
kwa kupanga ba kufanikisha mikakati mbalimbali, ambapo nilikutana nae Big
Brother mwanzoni mwa Mwaka huu, alikuwa anatoka PACIFIC HOTEL akaniambia kuwa
ametoka MBOZI MAGHARIBI ambako alikwenda kuchunguza kama DAVID SILINDE
anakubalika jimboni kwake, na hata ilipotokea sakata lililopelekea Mimi na
SHONZA na wengineo kuondoka Chadema, LUDOVICK ndiye mtu aliyetumwa kwenda MBEYA
akiwa na maagizo kutoka kwa DR SLAA ya kumfukuza UANACHAMA baba yangu Mzazi
(MZEE MWAMPAMBA ambae nae alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA) na ndiye aliyekuja
hapa jamiiforums (JF) kuweka post yenye barua za kufukuzwa kwa Mzee Mwampamba.
PAMOJA NA HAYA YOTE NA MENGINE AMBAYO AMEIFANYIA CHADEMA AMBAYO MIMI SIYAJUI,
VIONGOZI WA CHADEMA WANAKANA KUMFAHAMU……….,INAHUZUNISHA..!
Nimeshtushwa sana na Taarifa nilizoziona kwenye vyombo vya habari, juu ya Dr
SLAA kukana kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia na kufanya nae kazi yeyote
NDUGU yangu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA.
Lakini si hilo tu bali pia Mawakili ambao wamewekwa na Chadema ambao idadi yao
ni watano, wakiwemo (katika mawakili hao) viongozi waandamizi wa Chadema
wamekana kumtambua LUDOVICK.,ni USALITI KIASI GANI HUU..?
Mawakili wote watano ambao ni:-
i) MABERE MARANDO-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
ii) ABDALLAH SAFARI-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
iii) NYARONYO KICHERE
iv) TUNDU LISSU-MNADHIMU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI
v) PETER KIBATALA
Kwanini wasigawanywe hawa au wote katika hawa hawamtetei LUDO..? ama kama si
hawa kwanini hawatafutwi mawakili wengine kwa ajili ya LUDO na badala yake
akaachwa anaangamia pamoja na kujitolea kote kuijenga na kuitetea Chadema,
pamoja na utiifu wote wa kuwalinda na kutunza siri za viongozi na siri za Chama
hicho.
ANGALIZO:
Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango
au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata
mkumbo na upepo wa mawazo yao.
Naomba vijana wenzangu mfikiri kwa kina juu ya haya yaliyompata LUDOVICK na
mjifikirie hatma yenu ndani ya chama na maisha katika ujumla wake.
CHANZO"
MTELA MWAMPAMBA/ FACEBOOK
No comments:
Post a Comment