Balozi wa CANADA nchini bwana,
Alexandre Leveque katikati, katika mkutano na waandishi wa habari hawapo
pichani, alipotembelea shirika la Under the Same Sun kwa lengo la kujionea
utendaji wake pamoja na kuzindua vipindi vya kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu
Albinisim, mradi ambao umefadhiliwa kwa ushirikiano wa serikali ya Canada kupitia
ubalozi wake nchini na shirika la Under the Same Sun. kushoto kwake ni
Mkurugenzi mtendaji wa(UTSS) Bi,Vicky Ntetema.
Balozi wa Canada nchini Bwana Alexandre
Leveque, akibonyeza kitufe akizindua vipindi vya kampeni Tambua Albinism inayotarajiwa
kuanza mwezi wa April, Jumla ya vipindi kumi na mbili vyenye urefu wa dakika
therathini, vya michezo wa radio na makala mchanganyiko zenye lengo la kuongeza uelewa wa jamii
kuhusu albinism kama hali ya kurithi na changamoto zinazowakabili watu wenye
albinism (WWA), vitarushwa katika radio za kijamii Sengerema Fm, Sibuka Fm, Faraja Fm, Fedeco Fm, Kahama Fm na Chemchemi Fm ziliopo kanda ya ziwa.
Balozi wa Canada nchini Bwana, Alexandre
Leveque akikabidhi mfano wa hundi ya USD 20,000 kwa mkugenzi mtendaji wa UTSS
Bibi Vicky Ntetema kushoto kwake ambazo zitasaidia kutekeleza kampeni hiyo
yenye lango la kuamamsisha jamii juu yamaswala ya Albinism vipindi
vitakavyorushwa hewani kwa mda wa miezi sita.
Vipindi viwili kwa mwenzi vya makala
mchanganyiko vitarushwa na (kurudiwa), kipindi kimoja cha mchezo wa radio kitarushwa
hewani mara moja kwa mwezi na (kurudiwa0 pia kutakuwa na jopo la majadiliano ya
moja kwa moja pamoja na mazungumzo kati ya WWA, na wataalam wa maswala
ya albinism sanjali na michango ya wasikilizaji wakaochangia kwa njia ya simu.
No comments:
Post a Comment