Thursday, 23 August 2012

"SABABU ZETU WAISLAM KUGOMEA SENSA HIZI HAPA ZIWAZIII.


Mwaka 1967 nyerere aliondosha kipengele cha dini ktk sensa ya wananchi wa Tanzania United Republic kwa Sababu ya Kuwa Kinaweza Kuleta Udini. Cha Ajabu..
1.Ofisi ya waziri mkuu inadai wakristo ni 45% waislam 35% Na hili limo kwenye Calender zinazotolewa na ofisi ya waziri mkuu.
2.TBC 1 Tar 26 April 2012 Imetangaza Hadharani takwimu zinazoonyesha wakristo ni 52% waislam 32%(Sijui Wametuhesabu lini?)
3. Bodi ya utalii imeonyesha katika Website yao wakristo ni 45% waislam 40% (taarifa ambayo wameitoa na kuedit Mwezi mmoja na zaidi kutoka leo baada ya waislam kutumia kama reference mpaka kwenye vyombo vya habari).
4. Wakatoliki tovuti yao (www.rc.net ) wanadai waislam ni 34%na wao ni 44%
(Unapaswa kujiuliza ni lini walituhesabu?).
5. Takwimu za nama hii zipo kwenye Ramani zile kubwa kabisa zinazoonyesha nchi yetu na zile ilizopakana nazo( Ukitaka kuamini nunua hizo ramani au hata angalia tu.)
6.Angalia na Wikipedia nazo zinavyochezea takwimu bila woga http://en.wikipedia.org/wiki/Tanzania#Religion

Takwimu hizi za uogo zmekuwa zki2miwa ktk uteuzi na maamuzi kama ilivyo elezwa kuwa tz haiwez kujiunga na jumuiya ya kiislamu ya OIC sababu raia wakristo ni wengi kuliko waislam.
KAMA ULIKUA HUJUI KWANINI WATU WANAGOMA BASI LEO UJUE. SIO KAMA TUNAPENDA TU UBISHI ILA TUNAJUA TUNACHODAI NA SABABU TUNAZO TENA ZA MSINGI." abubakar

Angalizo: Nimekuwa nikijiuliza juu ya hili swala mda tangu kuibuka kwake ivyo nimeona kuna aja ya kupost hoja ya Abubakar na watanzania wote tuisome kisha tuchangie, lengo ni kueleweshana hata kukosoana ila zitumike lugha nzuri tafadhali wadau!


Sunday, 19 August 2012

Familia za wachimba migodi waliouliwa na polisi wa Afrika Kusini, wakati wa mgomo wa Alhamisi, zimekuwa zikipita mahospitali kuwatafuta jamaa zao.


Wake wa wachimba migodi wanasema polisi na mameneja wa kampuni ya mgodi hawakuwapa orodha ya wachimba migodi 34 waliouwawa na wengine wengi waliojeruhiwa kwenye mapambano hayo.
Polisi wanasema sasa wanashirikiana na mameneja wa mgodi kutoa orodha kuu, lakini haiwezi kufichua majina ya wachimba migodi zaidi ya 200 waliokamatwa.
Rais Jacob Zuma ametangaza kuwa ataunda tume ya kuchunguza mauaji hayo.
Rais wa chama cha wafanyakzi kisichokuwa rasmi, ameiambia BBC kwamba wanataka tume ya kimataifa na iliyo huru.
Polisi wanasema watu thelathini na wanne waliuwawa katika tukio hilo.
Rais wa chama cha wafanyakazi ambacho siyo rasmi, Joseph Mathunjwa, wa Association of Mineworkers and Construction Union, amesema kuwa wanataka tume huru ya kimataifa kuchunguza mauaji hayo kwa sababu chama chake tayari kinalaumiwa kwa ghasia hizo.
Kampuni inayomiliki migodi hiyo, Lonmin, imeahidi kusaidia familia za walioathirika, lakini inashikilia kuwa mgomo huo haukuwa halali.
Chama hicho kinataka nyongeza ya mshahara wa zaidi ya dola 1,000 kwa mwezi.
Watu kumi wakiwemo polisi wawili waliuwawa kabla ya tukio la siku ya Alhamisi.
 Source Bbc

Ugonjwa wa Ebola waibukia kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.


Wagonjwa wawili wamethibitishwa kuwa na virusi, mmoja wao amefariki.
Shirika la matibabu la MSF, lenye watu wake Isiro, linasema hatua zinachukuliwa ili kumtafuta na kumtenga mtu yeyote ambaye aliwakaribia wale walioambukizwa.
MSF katika taarifa yake inasema aina ya virusi vya Ebola ya Congo ni tofauti na ile ya Uganda, ambayo iliuwa watu 16 mwezi uliopita.
Sorce Bbc 

Nawatakia Waumini wa Dini Ya kiislam Sikuku njema ya Eid Mubarak



Eid Mubarak

Ukahaba wa kutisha waibuka Kigamboni Dar es Salaam

Source Mwananchi:

YUMKINI, wengi wanaposikia neno hili Loliondo akili zinaweza kuhamia kwa Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapila, maarufu kama Babu aliyepata umaarufu mwaka jana kwa kutibu maradhi mengi kwa dawa ya mitishamba iliyo katika kikombe.

 Lakini, Loliondo inayozungumziwa hapa si hiyo ya Babu wa Loliondo mkoani Arusha. Loliondo hii haina kikombe cha babu wala haitibu kwa mitishamba, bali ni eneo lililopo katika Kijiji Kichangani eneo la Kigamboni lenye upekee, likiwa umbali wa kilomita 40 kutoka katikati ya Jiji la Dar  es Salaam.

Upekee wake huo unatokana na majaliwa ya  ardhi yenye rutuba tele na uoto wa asili, lakini pia Kijiji cha Kichangani lilipo eneo la Loliondo lina mchanganyiko wa watu wa makabila zaidi ya matatu, asilimia 70 wakiwa ni Wasukuma.
 

Eneo hili lipo katika Kata ya Mbutu iliyopo Manispaa ya Temeke.

Baada ya kuvuka bahari kwa kutumia kivuko kutoka eneo la Kivukoni, yapo magari mengi  yanayoweza kukufikisha huko, ambayo wapigadebe wake hunadi maeneo maarufu wanayopita na utawasikia wapigadebe hao wakiita abiria " Mbutu- Kikwajuni – hadi Kichangani."

Ukishuka kituo cha mwisho wa gari, kinachoitwa Mbutu Kichangani, ukimuuliza hata mtoto mdogo Loliondo ni wapi hapa? Atakupeleka.

 Upekee mkubwa wa Loliondo ni kushamiri kwa biashara ya ukahaba, inayofanywa na wasichana wa  kuanzia umri wa miaka 13.

Loliondo ina nyumba zilizobatizwa jina la ‘ubanda’ na wenyeji wa eneo wakimaanisha vibanda. Nyumba hizo ndimo inapofanyika biashara hiyo pamoja na biashara ya kuuza pombe haramu ya gongo na bangi.
 

Wanawake wanaofanya biashara hiyo hapo Loliondo huitwa ‘wanawake wa ubanda’

Kwa nini eneo hilo likaitwa Loliondo?

Jina hilo linatokana na wanawake wanaotoa huduma ya ngono kuwaambia wanaume wanaotaka kupata huduma yao: “Ngoja nikapate kikombe cha Babu Loliondo."

Ndipo jina hilo lilizaliwa na kutumiwa zaidi ya wanaume hao, wakijaribu kutumia lugha ya kificho kwa safari ya kwenda huko, hata baadaye likakubalika na kuwa maarufu.

 Hamis Kashindye  ni mkazi wa Kichangani, Loliondo, kwa miaka 16 sasa, anasema kuwa kama ingepitishwa sensa kujua idadi ya wanawake wanaouza miili yao, basi wangeweza kuwa ni nusu ya wakazi wa eneo hilo.

 Anasema kuwa wanawake hao wanaofanya biashara ya ukahaba baadhi ni wakazi wa kudumu wa eneo hilo na wahamiaji kutoka maeneo ya Mbagala na Ilala.

“Hapa yapo mengi sana,(akimaanisha wanawake wanaojiuza) na kila siku yanaongezeka.  Wengine hawayapendi, lakini mimi naona yanasaidia sana,” anasema Kashindye  kwa lafudhi ya Kisukuma.

 Anaitetea kauli yake kwa kueleza kuwa wapo wanaume wasioweza kutongoza wanawake, hivyo wanarahisishiwa kazi kwa kutumia fedha zao kibindoni.

Anasema kuwa wanawake hao huwalenga wavuvi na wakulima wengine wa eneo hilo, ambao baada ya kupata fedha zao huzitumia kwa starehe.

 “Kama wavuvi na wakulima wa hapa wakishapata hela, wanamaliza hata Sh100,000 kwa hao wanawake wa ubanda,” anasema Kashindye akifafanua kuwa baadhi ya wanawake hao wana tabia ya kuha
ma hama wakifanya