Wake wa wachimba
migodi wanasema polisi na mameneja wa kampuni ya mgodi hawakuwapa orodha ya
wachimba migodi 34 waliouwawa na wengine wengi waliojeruhiwa kwenye mapambano
hayo.
Polisi wanasema sasa
wanashirikiana na mameneja wa mgodi kutoa orodha kuu, lakini haiwezi kufichua
majina ya wachimba migodi zaidi ya 200 waliokamatwa.
Rais Jacob Zuma
ametangaza kuwa ataunda tume ya kuchunguza mauaji hayo.
Rais wa chama cha
wafanyakzi kisichokuwa rasmi, ameiambia BBC kwamba wanataka tume ya kimataifa
na iliyo huru.
Polisi wanasema watu
thelathini na wanne waliuwawa katika tukio hilo.
Rais wa chama cha
wafanyakazi ambacho siyo rasmi, Joseph Mathunjwa, wa Association of Mineworkers
and Construction Union, amesema kuwa wanataka tume huru ya kimataifa
kuchunguza mauaji hayo kwa sababu chama chake tayari kinalaumiwa kwa ghasia
hizo.
Kampuni inayomiliki
migodi hiyo, Lonmin, imeahidi kusaidia familia za walioathirika, lakini
inashikilia kuwa mgomo huo haukuwa halali.
Chama hicho kinataka
nyongeza ya mshahara wa zaidi ya dola 1,000 kwa mwezi.
Watu kumi wakiwemo
polisi wawili waliuwawa kabla ya tukio la siku ya Alhamisi.
No comments:
Post a Comment