Tuesday, 19 February 2013

POLISI YAFANIKISHA KUKAMATWA KWA WAHALIFU KADHAA NA VIELELEZO MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM



Jeshi la polisi  kanda maalumu ya Dar es salaam limejipanga vema kupambana na uharifu unaosababishwa na vikundi vya watu wachache wanaotumia mwamvuli wa siasa na udini kwa lengo la kuvuruga amani jijini Dar es salaam na mikoa mingine nchini Tanzania.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema hivi karibuni katika vurugu za kidini zinazoendela nchini jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 91 na baada ya mchujo watuhumiwa 59 wamefikishwa mahakamani.


Sambamba na kukamata watuhumiwa hao, jeshi la polisi limefanikiwa kukamata dawa za kulevya, magari manne ambayo ni Toyota Daihatsu yenye namba za usajiri T 679 AZS, Toyota Colona T 212 ABB, Toyota vitz T 112 BND na Toyota Rav 4 T259 BSS
Vifaa vingine vilivyokamatwa katika msako huo ambao umehusisha mikoa yote ya kipolisi Mkoa wa Dar es salaam ni vifaa vya kuvunjia vioo vya magari, noti bandia za shilingi elfu kumi zenye thamani ya shilingii 270,000.

picha za chini ni baadhi magari yaliyokamatwa katika msako ulioendeshwa na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam










Thursday, 3 January 2013

TATHMINI NA MWELEKEO WA MVUA NCHINI KWA KIPINDI CHA JANUARI HADI MACHI, 2013

TAARIFA KWA UMMA      

A:  TATHMINI NA MWELEKEO WA MIFUMO YA HALI YA HEWA 
                                    JANUARI HADI MACHI 2013.
Katika kipindi cha mwezi Januari  hadi Machi  2013, hali ya joto la bahari katika ukanda wa tropikali ya mashariki na magharibi mwa bahari ya Pasifiki inatarajiwa kuwa ya wastani hadi chini ya wastani. Hali kadhalika, joto la bahari katikati ya bahari ya Hindi linatarajiwa kuwa chini ya wastani wakati joto la bahari karibu na pwani ya Tanzania linatarajiwa kuwa la wastani hadi juu ya wastani. Hali hii inatarajiwa kusababisha upepo wenye unyevunyevu kuvuma kutoka bahari ya Hindi kuelekea katika maeneo ya ukanda wa Pwani. Vilevile, joto la bahari katika bahari ya Atlantiki, kusini magharibi mwa bara la Afrika linatarajiwa kuwa la chini ya wastani na hivyo kusababisha upepo kutoka magharibi kuvuma kuelekea maeneo ya kusini magharibi mwa nchi. 

B: MWELEKEO WA MVUA KWA MWEZI JANUARI HADI MACHI  2013 
Mvua kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi, 2013 zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani, isipokuwa maeneo ya kaskazini magharibi  ambayo yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani. Aidha mchanganuo wake ni kama ifuatavyo; 

Maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua (Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki ukanda wa ziwa Victoria):

Baadhi ya maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka (Mikoa ya Dar es salaam, Tangam Pwani, Arusha, Kilimnjaro, Manyara, Mwanza, Mara, Geita, Shinyanaga, Kagera na Simiyu) yanatarajiwa kupata mwendelezo wa mvua (out of season rains) mwezi Januari.  Aidha utabiri wa mvua za masika katika maeneo haya utatolewa mwezi Februari, 2013.

 Mvua za Msimu
Kipindi cha mvua za Msimu Novemba hadi Aprili ni mahsusi kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka (Kanda ya Magharibi, Kanda ya kati, Nyanda za juu kusini magharibi, mikoa ya kusini na pwani ya kusini). Mvua zinaendelea kunyesha na kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2013 zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo;

Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani. 

Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma):
Mvua zinatarajiwa kuwa za  wastani hadi juu ya wastani. 

Nyanda za juu Kusini Magharibi: (Mbeya, Rukwa, Iringa na Morogoro-kusini ):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani.

Kanda ya kusini na Pwani ya kusini (Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu wastani. 

MUHIMU: Aidha katika maeneo mengi ya nchi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa viwango vya mvua ya wastani vinaendelea kushuka, hivyo kufanya mvua za wastani katika baadhi ya maeneo kutokidhi mahitaji ya shughuli mbali mbali kama vile kilimo, maji na nishati.

Taarifa inaonyesha kwa mfano maeneo ya kusini uwezekano wa kupata mvua za juu ya wastani ni asilimia arobaini 40%,  mvua za wastani 35% na mvua za chini ya wastani 25%.

D: ATHARI NA USHAURI
Kipindi cha mvua kilichobaki ni kifupi hivyo pamoja na matarajio ya mvua za wastani hadi juu ya wastani katika baadhi ya maeneo ya kati na kusini mwa nchi tunashauri maji yatumike kwa uangalifu hasa shughuli za umwagiliaji katika maeneo ya mito inayotiririsha maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ili kuwa na uhakika wa kupata maji ya kutosha katika mabwawa. Aidha vyanzo vya mito hiyo  (cathment areas) vihifadhiwe na kuhakikisha hakuna uharibifu wa mazingira.
Kuna uwezekano wa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa zinazoambatana na upepo mkali katika kipindi hiki cha mvua hivyo tahadhari ziendelee kuchukuliwa ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao.Tunashauri pia wafugaji wajenge tabia ya kuhifadhi malisho kwaajili ya kutumia wakati kunapokuwa na upungufu wa malisho.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania Itaendelea kufuatilia Mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na vimbunga katika bahari ya Hindi na kutoa taarifa kuhusiana na mwelekeo wa mvua nchini.

                 Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania


TCRA YATOA UFAFANUZI JUU YA CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA BAADA YA KUZIMA MITAMBO YA ANALOJIA DEC 31 DAR


Mkurugenzi wa TCRA Prof, John Nkoma akielezea changamoto zilizojitokeza kufatia kuzimwa kwa mitambo ya Analojia mapema Disemba 31 mwaka jana na kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa kurusha matangazo wa Dijitali katika jiji la Dar es salaam. Changamoto kubwa ni Kukatika kwa matangazo, kutokuwepo kwa baadhi ya stesheni katika baadhi ya ving'amuzi.


Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano (TCRA), Bwana Innocent Mungy  akitoa Samsung Min-Lap Top Kwa Bwana, Emmanuel Shayo mkazi wa Dar es Salaam, mmoja kati ya washindi wa zawadi kutoka TCRA kuatia kujibu maswali live mahojiano ya TBC1 juu ya kuzimwa kwa mitambo ya Analojia Kwenda Dijitali jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2012. Zoezi makabidhiano ulifanyika katika Towers Mawasiliano jijini Dar es Salaam jana. (Picha na hisani ya TCRA)


Mkuu wa Kitengo Cha mawasiliano (TCRA) Bwana,Innocent Mungy akimkabidhi Bi Amina Mandawa kutoka Kihonda, Morogoro,zawadi ya simu Nokia Asha 201 kutoka TCRA kuatia kujibu maswali live mahojiano ya TBC1 juu ya kuzimwa kwa mitambo ya Analojia Kwenda Dijitali jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2012. Zoezi makabidhiano ulifanyika katika Towers Mawasiliano jijini Dar es Salaam jana. (Picha na hisani ya TCRA)





Sunday, 30 December 2012

TAARIFA YA NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA MHE. JANUARY Y. MAKAMBA (MB), KUHUSU USITISHAJI WA MATANGAZO YA ANALOJIA NA KWENDA KATIKA MFUMO WA DIJITALI

Ndugu Wananchi,

Mtakumbuka kuwa hapo tarehe 23 Februari 2012 tuliwatangazia kupitia vyombo vya habari juu ya usitishwaji wa matangazo ya televisheni kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo mpya unaotumia teknolojia ya dijitali.


Napenda kuwaleleza kuwa, maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia kuanzia tarehe 31 Desemba 2012 yamekamilika kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Hata hivyo, napenda sasa kutoa taarifa kuwa uzimaji wa mitambo ya analojia utafanyika kwa awamu kama ifuatavyo:-

(1) Dar Es Salaam-31 Desemba, 2012;
(2) Dodoma & Tanga- 31 Januari, 2013;
(3) Mwanza-28 Februari, 2013;
(4) Moshi & Arusha-31 Machi, 2013;
(5) Mbeya-30 Aprili, 2013.


Tumeamua kuanza kuzima mitambo hiyo kwa Jiji la Dar es Salaam kwanza ili kutoa fursa kwa makampuni yenye leseni kusimika mitambo ya utangazaji wa dijitali katika mikoa mingine. Makampuni haya yamejipanga kukamilisha usimikaji wa mitambo hiyo katika mikoa minane katika miezi minane ijayo.

Mitambo ya analojia itakayozimwa kesho ni ile iliyopo Kisarawe na Makongo. Vituo ambavyo siku ya tarehe 1 Januari 2013, vitapaswa kuanza kutangaza matangazo kwa mfumo wa dijitali ni TBC1, ITV, EATV, Channel 10, StarTV, DTV, CapitalTV, TumainiTV, ATN, MlimaniTV, C2C, CTN, CloudsTV na Efatha.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inafanya jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba makampuni yenye leseni za kusambaza ving’amuzi yanakuwa na ving’amuzi vya kutosha na vingine vimeagizwa ili kukidhi mahitaji ya baadaye na vile vilivyopo sokoni vina ubora unaokubalika.

Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itahakikisha kwamba zoezi la uhamaji linafanyika bila usumbufu na kero kwa wananchi. Makampuni yanayouza ving’amuzi yameagizwa yaimarishe huduma kwa wateja wakati wa kuuza ving’amuzi na hata baada ya ununuzi iwapo wananchi watakuwa na matatizo na ving’amuzi.

Zoezi hili la uhamaji ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Tutakapokuwa tumekamilisha uhamaji, huduma za mawasiliano na utangazaji zitapanuka na kuwa bora zaidi. Kwa mfano, itawezekana sasa kuangalia televisheni kupitia simu zetu za mikononi. Vilevile, itawezekana, kwa bei nafuu kabisa, kwa mtu mwenye uwezo wa kutengeneza vipindi kukodisha chaneli yake na kutangaza vipindi vyake. Vilevile, bei za mawasiliano na utangazaji zitashuka, na tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye mapinduzi ya teknolojia duniani, ambayo nchi yetu haiwezi kubaki nyuma.

Ndugu Wananchi,

Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhamaji huu. Serikali inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya teknolojia ya analojia.

Uhamaji huu hautahusu televisheni za wananchi zinazopata matangazo kupitia madishi (nyungo) (satellite) au nyaya (cables). Hivyo, wananchi wanaopata matangazo kupitia DStv, Zuku, na nyinginezo wataendelea kupata matangazo yao kama kawaida.

Ndugu Wananchi

Kama kuna mwananchi yoyote ana kero, malalamiko, swali au anahitaji maelekezo kuhusu uhamaji, awasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia namba 0784-558270; 0784558271 au barua pepe: malalamiko@tcra.go.tz


Friday, 28 December 2012

RICHIE MAVOKO NA DAYNA WATOA SHUKRANI ZAO KWA WATANZANIA KWA KUWAPOKEA VIZURI MWAKA 2012.


Msanii Richie Mavoko pichani (katikati), Dayna kushoto kwake na Meneja wa sasa wa Richie Mavoko Bwana Rama a.k.a Papa Misifa, mda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini dar es Salaam.


Richie Mavoko akifafanua jambo katika mkutano wake na waandishi wa habari leo, ambapo alitoa shukrani zake kwa watanzania kwa kumpokea vizuri hasa kazi zake katika mwaka huu wa 2012 na kuahidi kuendelea kutoa nyimbo nzuri zaidi na zenye kuelimisha jamii.


Pamoja na mafaikio yake katika mwaka huu wa 2012, Richie Mavoko amewataja baadhi ya waliochangia kufikia mafanikio hayo kuwa ni pamoja na meneja wake wa zamani Bwana Maneno, Pia kampuni ya AL-JAZERRA ENTERTAINMENT, kwani ndio waliokiona kipaji chake na kumsaidia pia kuinua vipaji vya wasanii wengine wengi nchini kama DIAMOND, Sam wa Ukweli, DAYNA na wengineo
.

Hapa wakishoo swanga Baada ya mkutano wao na waandishi wa Habari, Dayna na Richie Mavoko

Monday, 24 December 2012

KAMPUNI YA SIMU YA TTCL YATOA MSAADA KWA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM


Meneja Mkuu wa TTCL kanda ya Dar es salaam Bwana,Charles Nkombelwe Akikabidhi msaada wenye samani ya zaidi Tsh 3 Mil, kwa mmoja wa wawakilishi wa vituo vya watoto kwa ajili ya kuwatakia maandlizi mema ya sikuku ya Krisimas na Mwaka mpya.


Msimamizi wa kituo cha Yatima Group Trust cha Tandika jijini Dar es Salaam, Akielezea furaha yake kufatia kuatiwa msaada huo kutoka TTCL.

Wawakilishi kutoka katika Vituo cha kulelea watoto yatima katika picha ya pamoja na baadhi ya msaada waliokabidhiwa na Kampuni ya Simu ya TTCL

TIGO YAZINDUA HUDUMA MPYA YA EXTREM PACK KUPITIA TIGO PESA.


Meneja Mauzo na Usabazaji wa Tigo Pesa Bwana Goodluck Charles wa kwanza kulia, akeleleza uzinduzi huo katika mkutano wa waandisha wa habari awapo pichani jijini Dar es salaam.


Afisa Masoko wa Tigo Bi, Jacqueine Nnunduma wa kwanza kushoto, Akitoa ufafanuzi juu ya huduma mpya ya Tigo ambapo amesema mteja wa Tigo atakaejiunga huduma hiyo ya XTREM kupitia akaunti yake ya Tigo Pesa atapata hapohapo mda wa nyongeza  wa Tsh 450 itayomwezesha kupiga simu mitandao yote nchini.


Afisa masoko wa Tigo Bi, Jacquein Nnundumawa kwanza kushoto, katikati Asisa Habari wa Tigo na Bwana Goodluck Meneja Mauzo na Usambazaji wa Tigo Pesa, wakimsikiliza kwa makini wakati akifafanua juu ya ukomo wa kifushi icho kuwa na saa 24 tangu kujinga,