CARDINAL JORGE MARIO BERGOGLIO KUTOKA NCHINI ARGENTINA ACHAGULIWA KUWA PAPA MPYA, NA KUCHAGUA JINA LA FRANCIS 1
Wednesday, 13 March 2013
Monday, 11 March 2013
POLISI WATANO WALIOHUSIKA NA WIZI WA MIL 150 WAFUKUZWA KAZI
Askari
watano SSGT Dancan, CPL Rajab, CPL Calvin, CPL Geofrey, na CPL kawanami
wamefukuzwa kazi kitokana na makosa mbalimbali ya kinidhamu pamoja na kuhusika
katika wizi wa Tsh 150 Milioni uliotokoea kariakoo tarehe 14 Dec mwaka jana.Akizungumza
na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam, Kamanda wa polisi kanda maalumu DCP
Sulemani Kova amsema, askari hao watashitakiwa kwa kumujibu na taratibu za
kijeshi ambapo zinataka askari yeyote kabla ya kushtakiwa mashtaka ya kiraia
wanatakiwa kushitakiwa katika mahakama za kijeshi kwanza.Kamanda
Kova ameongeza kuwa sambamba na kufukuzwa kazi jarada lao tayali limeshapelekwa
katika ofisi ya DPP na ofisi ya
mwanasheria wa serikali ili waweze kulipitia na kuona kama kuna uwezekano wa
washtakiwa hao kufikishwa katika mahakama za kawaida (Criminal Justice).
Pia Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanya Operetion ya kushtukiza jijini Dar es saaam, Na kufanikiwa kukamata Noti bandia za Elfu kumi Sita, Bastora iliyokuwa na risasi nane, Pikipiki aina ya Boxer yenye namba ya usajili T 639 CDS pamoja na watuhumiwa watau, lita 66 za pombe aina ya gongo, bangi, katika operation hiyo jeshi ilo likifanikiwa kuwakamta watuhumiwa 35 kutokana na makosa hayo.
MOAT KUZIMA MATANGAZO YA TV NCHINI
Chama
cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini MOAT, kimeiomba serikali kurudisha
mfumo wa kurusha matangazo ya anlojia kwa mda nchini kwani mfumo wa
dijitali unawanyima wananchi wengi haki ya ya kikatiba ya kupata
habari nchiniMwenyekiti
wa MOAT, Bwana Reginard Mengi amesema tangu kuanza kwa mfumo huo wa kurusha
matangazo wa dijitali nchi desemba31 mwaka jana, watu wengi hasa wa kipato cha
chini nchini wamekuwa wakishinshindwa kupata haki yao ya kikatiba ya kupata
habari ivyo kusababisha vituo vingi vya
kurusha matangazo ya tv kushindwa kufikia malengo yao kiutendaji.Ameongeza
kuwa ktk kipindi icho chote kuanzia desemba 31 mwaka jana ambapo mfumo wa
utangazaji wa analojia ulizimwa nchini na kuanza kutumika mfumo wa dijitali
kumepelekea wadhamini wengi kusitisha matangazo yao au kuyapeleka ktk radio
kutokana na kutokuwa na watazamaji wengi nchini wa tv, kwani wanaoweza kumiliki
mfumo huo mpya wa dijitali.Aidha
Bwana Mengi amebainisha kuwa kutokana na wadhamini wengi kusitisha kutoa
matangazo yao kutapelekea vituo vya
kurusha matangazo ya tv vingi nchini kushindwa kujiendesha au kusitisha kurusha
matangazo yake mda sio mrefu.
Tuesday, 19 February 2013
MBATIA ATOA USHAURI JUU YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Mwenyekiti wa chama cha NCCR
Mageuzi James Mbatia Katika kikao chake na wandishi wa habari jijini Dar es
salaam leo, Kufuatia matokea mabaya ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika
mwaka jana, chama cha NCCR Mageuzi kimemtaka rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Jakaya Kikwete kuunda tume itakayochunguza ubora wa elimu nchini.
amesema elimu ya Tanzania
inaporomoka kutokana na viongozi wa kuendekeza mambo ya kisisana na kuacha
mambo ya msingi ambayo ni ukombozi wa taifa.
Sambamba na hilo kimewataka
wabunge kuondoa tofauti zao za kisiasa na udini ili kujenge elimu ya Tanzania
ambayo kwa sasa inaelekea pabaya kama hatua za makusudi hazitachukuliwa
kunusuru ubora na mazingira ya ufundishaji katika shule za msingi na sekondari.
POLISI YAFANIKISHA KUKAMATWA KWA WAHALIFU KADHAA NA VIELELEZO MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM
Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limejipanga
vema kupambana na uharifu unaosababishwa na vikundi vya watu wachache
wanaotumia mwamvuli wa siasa na udini kwa lengo la kuvuruga amani jijini Dar es
salaam na mikoa mingine nchini Tanzania.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es salaam leo, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es
salaam Suleiman Kova amesema hivi karibuni katika vurugu za kidini zinazoendela
nchini jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 91 na baada ya mchujo
watuhumiwa 59 wamefikishwa mahakamani.
Sambamba na kukamata
watuhumiwa hao, jeshi la polisi limefanikiwa kukamata dawa za kulevya, magari
manne ambayo ni Toyota Daihatsu yenye namba za usajiri T 679 AZS, Toyota Colona
T 212 ABB, Toyota vitz T 112 BND na Toyota Rav 4 T259 BSS
Vifaa vingine vilivyokamatwa
katika msako huo ambao umehusisha mikoa yote ya kipolisi Mkoa wa Dar es salaam ni
vifaa vya kuvunjia vioo vya magari, noti bandia za shilingi elfu kumi zenye
thamani ya shilingii 270,000.
picha za chini ni baadhi magari yaliyokamatwa katika msako ulioendeshwa na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam
Thursday, 3 January 2013
TATHMINI NA MWELEKEO WA MVUA NCHINI KWA KIPINDI CHA JANUARI HADI MACHI, 2013
TAARIFA KWA UMMA
A: TATHMINI NA MWELEKEO WA MIFUMO YA HALI YA HEWA
JANUARI HADI MACHI 2013.
Katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2013, hali ya joto la bahari katika ukanda wa tropikali ya mashariki na magharibi mwa bahari ya Pasifiki inatarajiwa kuwa ya wastani hadi chini ya wastani. Hali kadhalika, joto la bahari katikati ya bahari ya Hindi linatarajiwa kuwa chini ya wastani wakati joto la bahari karibu na pwani ya Tanzania linatarajiwa kuwa la wastani hadi juu ya wastani. Hali hii inatarajiwa kusababisha upepo wenye unyevunyevu kuvuma kutoka bahari ya Hindi kuelekea katika maeneo ya ukanda wa Pwani. Vilevile, joto la bahari katika bahari ya Atlantiki, kusini magharibi mwa bara la Afrika linatarajiwa kuwa la chini ya wastani na hivyo kusababisha upepo kutoka magharibi kuvuma kuelekea maeneo ya kusini magharibi mwa nchi.
B: MWELEKEO WA MVUA KWA MWEZI JANUARI HADI MACHI 2013
Mvua kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi, 2013 zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani, isipokuwa maeneo ya kaskazini magharibi ambayo yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani. Aidha mchanganuo wake ni kama ifuatavyo;
Maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua (Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki ukanda wa ziwa Victoria):
Baadhi ya maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka (Mikoa ya Dar es salaam, Tangam Pwani, Arusha, Kilimnjaro, Manyara, Mwanza, Mara, Geita, Shinyanaga, Kagera na Simiyu) yanatarajiwa kupata mwendelezo wa mvua (out of season rains) mwezi Januari. Aidha utabiri wa mvua za masika katika maeneo haya utatolewa mwezi Februari, 2013.
Mvua za Msimu
Kipindi cha mvua za Msimu Novemba hadi Aprili ni mahsusi kwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka (Kanda ya Magharibi, Kanda ya kati, Nyanda za juu kusini magharibi, mikoa ya kusini na pwani ya kusini). Mvua zinaendelea kunyesha na kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2013 zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo;
Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Tabora, Katavi na Kigoma):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani.
Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani.
Nyanda za juu Kusini Magharibi: (Mbeya, Rukwa, Iringa na Morogoro-kusini ):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani.
Kanda ya kusini na Pwani ya kusini (Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu wastani.
MUHIMU: Aidha katika maeneo mengi ya nchi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa viwango vya mvua ya wastani vinaendelea kushuka, hivyo kufanya mvua za wastani katika baadhi ya maeneo kutokidhi mahitaji ya shughuli mbali mbali kama vile kilimo, maji na nishati.
Taarifa inaonyesha kwa mfano maeneo ya kusini uwezekano wa kupata mvua za juu ya wastani ni asilimia arobaini 40%, mvua za wastani 35% na mvua za chini ya wastani 25%.
D: ATHARI NA USHAURI
Kipindi cha mvua kilichobaki ni kifupi hivyo pamoja na matarajio ya mvua za wastani hadi juu ya wastani katika baadhi ya maeneo ya kati na kusini mwa nchi tunashauri maji yatumike kwa uangalifu hasa shughuli za umwagiliaji katika maeneo ya mito inayotiririsha maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ili kuwa na uhakika wa kupata maji ya kutosha katika mabwawa. Aidha vyanzo vya mito hiyo (cathment areas) vihifadhiwe na kuhakikisha hakuna uharibifu wa mazingira.
Kuna uwezekano wa kuwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa zinazoambatana na upepo mkali katika kipindi hiki cha mvua hivyo tahadhari ziendelee kuchukuliwa ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao.Tunashauri pia wafugaji wajenge tabia ya kuhifadhi malisho kwaajili ya kutumia wakati kunapokuwa na upungufu wa malisho.
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania Itaendelea kufuatilia Mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa pamoja na vimbunga katika bahari ya Hindi na kutoa taarifa kuhusiana na mwelekeo wa mvua nchini.
Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
TCRA YATOA UFAFANUZI JUU YA CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA BAADA YA KUZIMA MITAMBO YA ANALOJIA DEC 31 DAR
Mkurugenzi wa TCRA Prof, John Nkoma akielezea changamoto zilizojitokeza kufatia kuzimwa kwa mitambo ya Analojia mapema Disemba 31 mwaka jana na kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa kurusha matangazo wa Dijitali katika jiji la Dar es salaam. Changamoto kubwa ni Kukatika kwa matangazo, kutokuwepo kwa baadhi ya stesheni katika baadhi ya ving'amuzi.
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano (TCRA), Bwana Innocent Mungy akitoa Samsung Min-Lap Top Kwa Bwana, Emmanuel Shayo mkazi wa Dar es Salaam, mmoja kati ya washindi wa zawadi kutoka TCRA
kuatia kujibu maswali live mahojiano ya TBC1 juu ya kuzimwa kwa mitambo ya Analojia Kwenda Dijitali jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2012. Zoezi makabidhiano
ulifanyika katika Towers Mawasiliano jijini Dar es Salaam jana. (Picha na
hisani ya TCRA)
Mkuu wa Kitengo Cha mawasiliano (TCRA) Bwana,Innocent Mungy akimkabidhi Bi Amina Mandawa kutoka Kihonda, Morogoro,zawadi ya simu Nokia Asha 201 kutoka TCRA kuatia kujibu maswali live mahojiano ya TBC1 juu ya kuzimwa kwa mitambo ya Analojia Kwenda Dijitali jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2012. Zoezi makabidhiano ulifanyika katika Towers Mawasiliano jijini Dar es Salaam jana. (Picha na hisani ya TCRA)
Subscribe to:
Posts (Atom)
