Thursday, 17 April 2014

KUTOKA NACTE KWENDA KWA WANAFUNZI WOTE WANAOTAKA KUJIUNGA NA VYUO MBALIMBALI,

Katibu Mtendaji wa NACTE Dokta Primus D Nkwera akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam BARAZA la Vyuo vya Ufundi nchini(NACTE) limesema Tatizo la Vyuo Feki halitakwisha Tanzania, kutokana na Vyombo vya Habari nchini kuhusika katika kuvitangaza vyuo hivyo. Hayo yalisemwa leo na Katibu Mtendaji wa NACTE Dokta Primus D Nkwera wakati wa mkutano na Waandishi Habari makao makuu baraza hilo jijini dar es Salaam,ambapo alisema tatizo la vyuo feki ambavyo havijasajiliwa havitakwisha kutokana na Vyombo vya Habari nchini kuzidi kuvitangaza. “Mimi nataka nikwambia tatizo hili la vyuo feki halitakwisha hapa nchini kutokana na vyombo vya Habari kuzidi kuvitanga vyuo hivi,leo ukiangalia kwenye television utaona kati ya matangazo nane ya vyuo yanoyotangazwa,kati ya hivyo vyuo vinne havijasajiliwa”alisema Nkwera Nkwera alizidi kusema wao walishakaa na Wahariri wa vyombo hivi vya Habari kuhusu kuvibana vyuo hivi. “Tulishakaa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari tuliambiwa eti suala hilo la watu wa masoko ndio wanahusika kwahiyo wao hayawahusu tena, huku wengine wakisema hawezi kufanya hivyo ”aliongeza Nkwera Hata Hivyo vyote ambavyo vitataka kuchukua wanafunzi wanoanza shahada ya cheti wanatakiwa kumchukua mwanafunzi aliyepata D mbili na E tatu ndiyo wanatakiwa kutumia badala ya mfumo wa Zamani wa D tatu. Katika hatua nyingine Baraza hilo limewataka wanafunzi wote wanaotaka kuomba mwaka wa masomo kwenye vyuo vya Afya nchini watumie njia ya mtandao. Akizungumzia hayo Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kutoka wizara wa Afya Dr Otilia Gowelee alisema kwa sasa wanafunzi wote ambao wanataka kuomba ngazi ya cheti na Diploma kwa sasa wanatakiwa kuomba kwenye mtandao. “Tunawaomba wanafunzi wote wanaotaka kuomba ngazi ya cheti au Diploma kwenye vyuo vya afya nchini wanatakiwa kuomba kupitia kwenye mtandao,kuliko utaratibu wa mwanzo,kwa sasa wanafunzi wanaweza kwenda kwenye mtandao wa NACTE,nakuanza kuomba”alisema Gowele Gowelee aliitaja miatandao ambayo wanatakiwa kutumia kuomba ambayo ni, www.nacte.go.tz, au www.moh.go.tz, www.cas.ac.tz Ikumbukwe kwa sasa Baraza hilo limevisajili vyuo 11 kwa mda wa wiki moja,na kwa sasa baraza hilo limewataka watu wote wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu kuanza kuomba kwa sasa maana Nafasi zimefunguliwa ziko wazi cha msingi uwe umefahulu kwa kiwango kizuri na mwisho wa kuomba nafasi hiyo ni 30 mwezi wa Sita

No comments:

Post a Comment