Sunday, 30 December 2012

TAARIFA YA NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA MHE. JANUARY Y. MAKAMBA (MB), KUHUSU USITISHAJI WA MATANGAZO YA ANALOJIA NA KWENDA KATIKA MFUMO WA DIJITALI

Ndugu Wananchi,

Mtakumbuka kuwa hapo tarehe 23 Februari 2012 tuliwatangazia kupitia vyombo vya habari juu ya usitishwaji wa matangazo ya televisheni kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo mpya unaotumia teknolojia ya dijitali.


Napenda kuwaleleza kuwa, maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia kuanzia tarehe 31 Desemba 2012 yamekamilika kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Hata hivyo, napenda sasa kutoa taarifa kuwa uzimaji wa mitambo ya analojia utafanyika kwa awamu kama ifuatavyo:-

(1) Dar Es Salaam-31 Desemba, 2012;
(2) Dodoma & Tanga- 31 Januari, 2013;
(3) Mwanza-28 Februari, 2013;
(4) Moshi & Arusha-31 Machi, 2013;
(5) Mbeya-30 Aprili, 2013.


Tumeamua kuanza kuzima mitambo hiyo kwa Jiji la Dar es Salaam kwanza ili kutoa fursa kwa makampuni yenye leseni kusimika mitambo ya utangazaji wa dijitali katika mikoa mingine. Makampuni haya yamejipanga kukamilisha usimikaji wa mitambo hiyo katika mikoa minane katika miezi minane ijayo.

Mitambo ya analojia itakayozimwa kesho ni ile iliyopo Kisarawe na Makongo. Vituo ambavyo siku ya tarehe 1 Januari 2013, vitapaswa kuanza kutangaza matangazo kwa mfumo wa dijitali ni TBC1, ITV, EATV, Channel 10, StarTV, DTV, CapitalTV, TumainiTV, ATN, MlimaniTV, C2C, CTN, CloudsTV na Efatha.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inafanya jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba makampuni yenye leseni za kusambaza ving’amuzi yanakuwa na ving’amuzi vya kutosha na vingine vimeagizwa ili kukidhi mahitaji ya baadaye na vile vilivyopo sokoni vina ubora unaokubalika.

Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itahakikisha kwamba zoezi la uhamaji linafanyika bila usumbufu na kero kwa wananchi. Makampuni yanayouza ving’amuzi yameagizwa yaimarishe huduma kwa wateja wakati wa kuuza ving’amuzi na hata baada ya ununuzi iwapo wananchi watakuwa na matatizo na ving’amuzi.

Zoezi hili la uhamaji ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Tutakapokuwa tumekamilisha uhamaji, huduma za mawasiliano na utangazaji zitapanuka na kuwa bora zaidi. Kwa mfano, itawezekana sasa kuangalia televisheni kupitia simu zetu za mikononi. Vilevile, itawezekana, kwa bei nafuu kabisa, kwa mtu mwenye uwezo wa kutengeneza vipindi kukodisha chaneli yake na kutangaza vipindi vyake. Vilevile, bei za mawasiliano na utangazaji zitashuka, na tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye mapinduzi ya teknolojia duniani, ambayo nchi yetu haiwezi kubaki nyuma.

Ndugu Wananchi,

Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhamaji huu. Serikali inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya teknolojia ya analojia.

Uhamaji huu hautahusu televisheni za wananchi zinazopata matangazo kupitia madishi (nyungo) (satellite) au nyaya (cables). Hivyo, wananchi wanaopata matangazo kupitia DStv, Zuku, na nyinginezo wataendelea kupata matangazo yao kama kawaida.

Ndugu Wananchi

Kama kuna mwananchi yoyote ana kero, malalamiko, swali au anahitaji maelekezo kuhusu uhamaji, awasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia namba 0784-558270; 0784558271 au barua pepe: malalamiko@tcra.go.tz


Friday, 28 December 2012

RICHIE MAVOKO NA DAYNA WATOA SHUKRANI ZAO KWA WATANZANIA KWA KUWAPOKEA VIZURI MWAKA 2012.


Msanii Richie Mavoko pichani (katikati), Dayna kushoto kwake na Meneja wa sasa wa Richie Mavoko Bwana Rama a.k.a Papa Misifa, mda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini dar es Salaam.


Richie Mavoko akifafanua jambo katika mkutano wake na waandishi wa habari leo, ambapo alitoa shukrani zake kwa watanzania kwa kumpokea vizuri hasa kazi zake katika mwaka huu wa 2012 na kuahidi kuendelea kutoa nyimbo nzuri zaidi na zenye kuelimisha jamii.


Pamoja na mafaikio yake katika mwaka huu wa 2012, Richie Mavoko amewataja baadhi ya waliochangia kufikia mafanikio hayo kuwa ni pamoja na meneja wake wa zamani Bwana Maneno, Pia kampuni ya AL-JAZERRA ENTERTAINMENT, kwani ndio waliokiona kipaji chake na kumsaidia pia kuinua vipaji vya wasanii wengine wengi nchini kama DIAMOND, Sam wa Ukweli, DAYNA na wengineo
.

Hapa wakishoo swanga Baada ya mkutano wao na waandishi wa Habari, Dayna na Richie Mavoko

Monday, 24 December 2012

KAMPUNI YA SIMU YA TTCL YATOA MSAADA KWA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM


Meneja Mkuu wa TTCL kanda ya Dar es salaam Bwana,Charles Nkombelwe Akikabidhi msaada wenye samani ya zaidi Tsh 3 Mil, kwa mmoja wa wawakilishi wa vituo vya watoto kwa ajili ya kuwatakia maandlizi mema ya sikuku ya Krisimas na Mwaka mpya.


Msimamizi wa kituo cha Yatima Group Trust cha Tandika jijini Dar es Salaam, Akielezea furaha yake kufatia kuatiwa msaada huo kutoka TTCL.

Wawakilishi kutoka katika Vituo cha kulelea watoto yatima katika picha ya pamoja na baadhi ya msaada waliokabidhiwa na Kampuni ya Simu ya TTCL

TIGO YAZINDUA HUDUMA MPYA YA EXTREM PACK KUPITIA TIGO PESA.


Meneja Mauzo na Usabazaji wa Tigo Pesa Bwana Goodluck Charles wa kwanza kulia, akeleleza uzinduzi huo katika mkutano wa waandisha wa habari awapo pichani jijini Dar es salaam.


Afisa Masoko wa Tigo Bi, Jacqueine Nnunduma wa kwanza kushoto, Akitoa ufafanuzi juu ya huduma mpya ya Tigo ambapo amesema mteja wa Tigo atakaejiunga huduma hiyo ya XTREM kupitia akaunti yake ya Tigo Pesa atapata hapohapo mda wa nyongeza  wa Tsh 450 itayomwezesha kupiga simu mitandao yote nchini.


Afisa masoko wa Tigo Bi, Jacquein Nnundumawa kwanza kushoto, katikati Asisa Habari wa Tigo na Bwana Goodluck Meneja Mauzo na Usambazaji wa Tigo Pesa, wakimsikiliza kwa makini wakati akifafanua juu ya ukomo wa kifushi icho kuwa na saa 24 tangu kujinga,