Tuesday, 19 February 2013

MBATIA ATOA USHAURI JUU YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia Katika kikao chake na wandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Kufuatia matokea mabaya ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana, chama cha NCCR Mageuzi kimemtaka rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kuunda tume itakayochunguza ubora wa elimu nchini.
amesema elimu ya Tanzania inaporomoka kutokana na viongozi wa kuendekeza mambo ya kisisana na kuacha mambo ya msingi ambayo ni ukombozi wa taifa.
Sambamba na hilo kimewataka wabunge kuondoa tofauti zao za kisiasa na udini ili kujenge elimu ya Tanzania ambayo kwa sasa inaelekea pabaya kama hatua za makusudi hazitachukuliwa kunusuru ubora na mazingira ya ufundishaji katika shule za msingi na sekondari.

 





POLISI YAFANIKISHA KUKAMATWA KWA WAHALIFU KADHAA NA VIELELEZO MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM



Jeshi la polisi  kanda maalumu ya Dar es salaam limejipanga vema kupambana na uharifu unaosababishwa na vikundi vya watu wachache wanaotumia mwamvuli wa siasa na udini kwa lengo la kuvuruga amani jijini Dar es salaam na mikoa mingine nchini Tanzania.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema hivi karibuni katika vurugu za kidini zinazoendela nchini jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 91 na baada ya mchujo watuhumiwa 59 wamefikishwa mahakamani.


Sambamba na kukamata watuhumiwa hao, jeshi la polisi limefanikiwa kukamata dawa za kulevya, magari manne ambayo ni Toyota Daihatsu yenye namba za usajiri T 679 AZS, Toyota Colona T 212 ABB, Toyota vitz T 112 BND na Toyota Rav 4 T259 BSS
Vifaa vingine vilivyokamatwa katika msako huo ambao umehusisha mikoa yote ya kipolisi Mkoa wa Dar es salaam ni vifaa vya kuvunjia vioo vya magari, noti bandia za shilingi elfu kumi zenye thamani ya shilingii 270,000.

picha za chini ni baadhi magari yaliyokamatwa katika msako ulioendeshwa na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam